Pata Elimu

Kwa hivyo, ugonjwa wa mboo kudinda kusimama (erectile dysfunction (ED)) ni nini?

Kwa kuona tu kichwa hiki, tayari unaangalia chini katika sehemu zako za siri kwa uoga, lakini huhitaji kuwa na wasiwasi wowote.

Zaidi ya asilimia 95 (95%) ya wanaume wanaougua ugonjwa wa mboo kudinda kusimama (erectile dysfunction (ED) wanaweza kutibiwa. Wanaume wengi huhofia wazo la kutoweza ‘kusimamisha’. Ukweli ni kwamba wakati fulani maishani mwako, hali hii imekutendekea au inaweza kukutendekea. Kulingana na utafiti wa hivi karibuni, kiwango cha kuenea kwa ugonjwa wa ED duniani kilikuwa asilimia 3 – 76.5%. Wakati mwingine kuwa na tatizo la kutoweza kusimamisha mboo si ugonjwa wa mboo kudinda kusimama. Ugonjwa wa ED unafafanuliwa kama kutoweza kusimamisha au kudumisha uthabiti wa mboo iliyosimama kwa kiwango cha kutosha kushiriki ngono.

[1] Centers for Disease Control and Prevention. Diabetes and Men. Accessed online: https://www.cdc.gov/diabetes/library/features/diabetes-and-men.html [2] National Library of Medicine. The global prevalence of erectile dysfunction: a review.
Accessed online: https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/31267639/#:~:text=Results%3A%20The%20global%20prevalence%20of,was%20positively%20associated%20with%20CVD.