Majibu na maswali

Una maswali? Usijali

Swali: Ni tofauti gani iliyopo kati ya ugonjwa wa mboo kudinda kusimama (erectile dysfunction (ED) na udhaifu/uhanithi (impotence)?

Jibu

Jibu Kwa kawaida, neno ED hutumiwa katika ufafanuzi wa aina mbalimbali za magonjwa yanayowakabili hasa wanaume – kama vile “kutoweza kusimamisha au kudumisha uthabiti wa mboo iliyosimama kwa kiwango kidogo wakati mwingine”1a. Kwa upande mwingine, udhaifu/uhanithi una maana mbaya zinazohusishwa na matumizi yake kwa sababu hutumiwa kama neno la jumla la kueleza matatizo ya wanaume kutokuwa na nguvu za kiume ambayo yanajumuisha kupungua kwa “hamu ya kushiriki ngono, kutoweza kufika kilele au kumwaga, na mboo kudinda kusimama”.

Swali: Ikiwa mwanaume anafikiri kuwa huenda ana ugonjwa wa mboo kudinda kusimama, anapaswa kumwona daktari wake wakati gani?

Jibu

Jibu Wakati mwingine kunaweza kuwa na visababishi fulani vya mawazo vinavyoweza kumsumbua mtu kwa sababu ya tukio fulani lililotendeka maishani mwake, ambavyo vinaweza kumfanya asiweze kusimamisha au kudumisha uthabiti wa mboo iliyosimama kwa muda. Katika hali hii, haimaanishi kuwa anahitaji kumwona mtoa huduma za afya mara moja. Hata hivyo, ikiwa hakuna tukio kama hilo lililotendeka na ugonjwa wa ED uwe tatizo sugu, basi anashauriwa azungumze na mtoa huduma za afya wa kuaminika ili kubainisha ni nini kinachoweza kuwa chanzo cha tatizo hilo

Swali: Je, dawa zitasababisha athari?

Jibu

Jibu Dawa zinaweza kutibu kila mtumiaji kwa njia tofauti na athari zake zinaweza kutofautiana kuanzia kwa athari ndogo hadi kali kiasi. Athari ndogo zinaweza kujumuisha kusokotwa na tumbo, kuumwa na kichwa na ngozi ya uso kubadilika kuwa nyekundu. Asilimia ndogo ya wanaume hukumbwa na hali ya matatizo ya kuona kwa muda baada ya kutumia baadhi ya dawa za kutibu ugonjwa wa ED

Swali: Je, kuna wanaume wowote ambao hawapaswi kutumia dawa hizo?

Jibu

Jibu Dawa za kutibu ugonjwa wa ED kwa kawaida hazishauriwi kutumiwa na wanaume walio na ugonjwa wa mshipa wa damu wa moyo kwa sababu dawa hizi zinaweza kusababisha shinikizo la damu ya wanaume kushuka hadi viwango hatari

Swali: Sikuwa nimewahi kusikia kuhusu ugonjwa wa ED hadi miaka kadhaa iliyopita. Je, ni ugonjwa mpya?

Jibu

Jibu Ingawa ugonjwa wa ED umekuwa mada nyeti kwa kiasi fulani, utafiti unaohusiana nao unaweza kupatikana kuanzia miaka ya mapema ya 1668 ambapo iligunduliwa kwamba sindano inaweza kutumiwa kusababisha mboo kusimama3a.Kwa sasa, matangazo na kampeni zimewezesha kufanya ugonjwa wa ED kuwa mada ya kuzungumziwa zaidi na kusababisha kuenezwa kwa uhamasisho zaidi kwa sababu wanaume wengi wanatafuta msaada kuhusu ugonjwa huu

Swali: Je, bado ninaweza kushiriki ngono ikiwa nina ugonjwa wa ED?

Jibu

Jibu Ndiyo, “mboo iliyosimama kama kawaida” si lazima kwa watu fulani kuishi maisha wanayoshiriki ngono

Swali: Je, kuna tiba zozote za ugonjwa wa ED au ni hali isiyoweza kutibiwa?

Jibu

Jibu Ugonjwa wa ED umechukuliwa kwa muda mrefu kuwa hali isiyoweza kutibiwa, lakini kwa miongo miwili iliyopita, kuongezeka kwa uhamasisho na elimu kumewezesha hali hiyo kuchukuliwa kama “ugonjwa wa kimwili unaoweza kutibiwa”. Matibabu ya ugonjwa wa ED yanaweza kutofautiana kuanzia kwa matumizi ya dawa au upasuaji hadi kwa kutambuliwa na kutibiwa kwa vyanzo vya msingi vya kisaikolojia na kihisia. Unapaswa kumwona mtoa huduma za afya wa kuaminika ili akusaidie kubainisha matibabu bora zaidi ya ugonjwa wako wa ED

Swali: Daktari wangu atatibu aje ugonjwa wa mboo kudinda kusimama?

Jibu

Kuna hali ya makubaliano inayozidi kuongezeka kuwa ugonjwa wa ED ni wa kimwili kwa kiwango kikubwa. Kwa hivyo, mtoa huduma wako wa afya anaweza kupendekeza mwanzoni kuwa utambue na kutibu vyanzo vya msingi vinavyoweza kuwepo vya kisaikolojia na kihisia. Mapendekezo haya yanaweza kujumuisha mabadiliko ya mtindo wa maisha, ushauri au uwezekano wa kubadilisha kanuni za matumizi ya dawa yoyote ambayo huenda unatumia

Swali: Ninawezaje kupimwa ili kutambua iwapo nina ugonjwa wa mboo kudinda kusimama?

Jibu

Jibu Hakuna vipimo maalum vya kutambua iwapo mtu ana ugonjwa wa ED. Hata hivyo, uchunguzi wa kimatibabu unaweza kufanywa kupitia sampuli fulani za damu na zaidi kupitia mazungumzo ambayo yanamhimiza mgonjwa kujitolea kutoa maelezo mengi kuhusu afya yake ya kisaikolojia na kihisia, na vigezo vya kijamii na demografia na mbinu zingine.

Swali: Mazoezi yanawezaje kutibu ugonjwa wa mboo kudinda kusimama?

Jibu

Jibu Imetambuliwa sana kuwa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara ni mojawapo ya vigezo muhimu zaidi vya kurekebisha hali hiyo, na kwa hivyo ni muhimu katika kutibu ugonjwa wa mboo kudinda kusimama. Mazoezi yanasemekana kuwa na ufanisi mkubwa yanapotumiwa pamoja na dawa kama ilivyoagizwa na mtoa huduma za afya wa kuaminika.

Swali: Je, ugonjwa wa mboo kudinda kusimama unaweza kusababisha utasa kwa mwanaume?

Jibu

Jibu Kuna vyanzo vingi ambavyo vinaweza kusababisha utasa kwa wanaume, njia ya msingi ya kupima ni kupitia uchanganuzi wa manii. Mtaalamu huchunguza wingi, hali ya kusonga na umbo la manii ili kuona ikiwa kuna hali zozote zisizo za kawaida katika uchanganuzi wa manii. Kwa hivyo, mwanaume anayeugua ugonjwa wa ED hawezi kuchukuliwa kuwa ni tasa isipokuwa uchanganuzi wa manii uonyeshe hali zisizo za kawaida7. Imetambuliwa kuwa ugonjwa wa ED unaweza kuwa na athari kwa uwezo wa mwanaume kuzalisha8kwa kuzuia uwezo wake wa kutungisha mwanamke mimba, hata hivyo, hali zote mbili si lazima ziambatane.

Swali: Ni tofauti gani iliyopo kati ya ugonjwa wa ED na ugonjwa wa kutoweza kumwaga?

Jibu

Jibu Ugonjwa wa mboo kudinda kusimama (erectile dysfunction) unafafanuliwa kama hali ya kutoweza kusimamisha na kudumisha uthabiti wa mboo iliyosimama1e. Ilhali ugonjwa wa kutoweza kumwaga (ejaculatory dysfunction) unafafanuliwa kama hali ya kutoweza kumwaga, kumwaga haraka sana au kuchelewa kumwaga

Swali: Je, ni lazima nipatwe na ugonjwa mboo kudinda kusimama kadri ninavyozidi kuwa mzee?

Jibu

Jibu Licha ya kuenea kwake kwa wanaume wazee, si lazima upatwe na ugonjwa wa ED kadri unapozidi kuwa mzee. Ugonjwa wa ED haubagui kulingana na umri na vyanzo vingi vya ugonjwa wa ED si lazima vihusiane na hali ya kuwa mzee. Ukweli halisi ni kwamba malalamiko kuhusu wanaume wenye umri mdogo kukumbwa na hali ya kushindwa kufanya kazi nzuri yanazidi kuongezeka: tafiti zinakadiria kwamba mmoja kati ya wagonjwa wanne wanaotafuta huduma za matibabu ya ugonjwa wa ED alikuwa na umri wa chini ya miaka 40.

Swali: Je, ugonjwa wa mboo kudinda kusimama unaweza kusababishwa na athari za dawa?

Jibu

Kwa ufupi – Ndiyo. Lakini lazima upate ushauri wa daktari wako kabla ya kuacha kutumia dawa yoyote. Daktari wako anaweza kukuandikia dawa tofauti, na dawa ya kutibu ugonjwa wa ED inapatikana kwa urahisi na ni salama kwa wanaume. Hali isiyofuata kanuni hii ni dawa fulani za ugonjwa wa moyo na viharusi, zinazojulikana kama naitreti/chumvi za kiasili ambazo hupanua mishipa ya damu iliyozibwa kwa wagonjwa wanaougua ugonjwa wa angina. Kwa bahati mbaya, naitreti/chumvi na tembe za kutibu ugonjwa wa ED hazichanganyiki, hali ambayo husababisha shinikizo la damu kupungua kwa viwango hatari ambavyo vinaweza kusababisha kifo12. Lakini, kuna njia zingine za kuweza kusimamisha mboo, kwa hivyo usipoteze matumaini yote ya kupata burudani kitandani.

[1] Erectile Dysfunction - FAQs | University of Maryland Medical Center. (n.d.). Retrieved February 8, 2022, from https://www.umms.org/ummc/health-services/urology/conditions-treatments/erectile-dysfunction/faqs [2] Chun, J. and Carson, C.C. (2001) “PHYSICIAN-PATIENT DIALOGUE AND CLINICAL EVALUATION OF ERECTILE DYSFUNCTION,” Urologic Clinics of North America, 28(2), pp. 249–258. doi:10.1016/S0094-0143(05)70135-X. [3] Jonas, U. (n.d.). The history of erectile dysfunction management. Retrieved February 8, 2022, from www.nature.com/ijir [4] Strahilevitz, J. et al. (2005) “An outbreak of Phialemonium infective endocarditis linked to intracavernous penile injections for the treatment of impotence,” Clinical Infectious Diseases, 40(6), pp. 781–786. doi:10.1086/428045/2/40-6-781-FIG001.GIF. [5] Blanker, M.H. et al. (2001) “Erectile and ejaculatory dysfunction in a community-based sample of men 50 to 78 years old: prevalence, concern, and relation to sexual activity,” Urology, 57(4), pp. 763–768. doi:10.1016/S0090-4295(00)01091-8. [6] Duca, Y. et al. (2019) “Erectile dysfunction, physical activity and physical exercise: Recommendations for clinical practice,” Andrologia, 51(5), p. e13264. doi:10.1111/AND.13264. [7] Infertility | Reproductive Health | CDC. (n.d.). Retrieved February 8, 2022, from https://www.cdc.gov/reproductivehealth/infertility/index.htm Erectile Dysfuncitona nd Infertility. In: J. P. Mulhall & W. Hsiao, eds. Men's Sexual Health and Fertility: A Clinician's Guide. London: Springer, p. 268. [9] Von Thesling-Sweet, G. & Shindel, A. W., 2014. Physiology of Erection. In: J. P. Mulhall & W. Hsiao, eds. Men's Sexual Health and Fertility: A Clinician's Guide. London: Springer, p. 268. [10] Otani, T. 2019.