Pata Elimu

Ni nini husababisha ugonjwa wa mboo kudinda kusimama?

Huenda hali hii imekutendekea, au huenda ulisikia rafiki akilalamika kwamba hakuweza ‘kufanya kazi nzuri’ kwa sababu alikuwa amekunywa pombe sana.

Ingawa hili linawezekana kabisa, kuna sababu zingine ambazo huenda zilisababisha ushindwe kufanya kazi nzuri. Hali ya mwanaume kusisimkwa kingono ni mchakato changamano ambao unahusisha sehemu nyingi za mwili kuliko jinsi unavyotarajia. Akili, homoni, hisia, neva, misuli na mishipa ya damu vyote huchangia. Wakati ambapo ni vigumu sana kusimamisha mboo kwa uthabiti kuliko jinsi inavyopaswa kuwa katika zaidi ya hali zisizo za kawaida, ni vyema ufanyiwe uchunguzi kwa sababu kwa kawaida ugonjwa wa ED unahusiana kwa ukaribu sana na hali ya afya ya mwili au kisaikolojia.

Uhusiano wa kichwa/moyo

Ugonjwa wa ED unaweza kuwa dalili ya onyo la mapema la ugonjwa wa moyo.Hata hivyo, ni utaratibu wa msingi: sehemu ya mwili ambayo hupiga damu mwilini inahitaji pia kusukuma damu ya ziada kwa kitu ambacho wanaume wengi huchukulia kuwa sehemu muhimu zaidi ya mwili wao kwa muda ili kudumisha uthabiti wa mboo iliyosimama.

Ikiwa kitu fulani kitakatiza mzunguko huu wa damu, basi mboo haitasimama. Neno la kimatibabu la kitu ambacho husababisha hali hii ni ‘atherosclerosis’, ambalo linamaanisha kuwa kuna uwezekano mishipa ya damu ya moyo wako imezibwa mahali fulani. Hali hizi za kuzibwa zinatokana na mkusanyiko wa utando wa mafuta. Utando wa mafuta huzuia mzunguko wa damu2. Matatizo ya mishipa ya damu ni mojawapo ya sababu kuu zinazosababisha ugonjwa wa ED2.

Habari njema ni kuwa kuna kitu kinachoweza kufanywa ili kuondoa hali hizi za kuzibwa – ukizitambua mapema; yaani, kabla hujapatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Kwa hivyo, kwa upande mwingine mzuri, ugonjwa wa ED unaweza kuokoa maisha yako kwa kutambua matatizo ya moyo na kutibiwa.

Haya yote yanatendeka kichwani?

Kinachotendeka kichwani mwako kinaweza kuathiri kazi yako kitandani. Utafiti unaonyesha kuwa hadi asilimia 20 (20%) ya visa vya ugonjwa wa ED ni vya kisaikolojia. Sababu zote za kisaikolojia zinazoweza kuwa na athari mbaya kwa maisha ya kingono zinajumuisha:

  • Msongo wa mawazo
  • Wasiwasi
  • Matatizo ya uhusiano
  • Unyogovu
  • Wasiwasi wa kutofanya kazi nzuri
  • Kujilaumu
  • Kiwango cha chini cha kujiamini

Kisha, kama vile ilivyo bahati mbaya, kuwa na wasiwasi kwamba hali hiyo huenda ikatokea tena, kunaweza kusababisha hali hiyo kutokea tena.

Akili yako ikiwa inasumbuliwa na mawazo yasiyofaa, mwili wako unaweza kutoa homoni (inayojulikana kama cortisol) ambayo hubana mishipa ya damu kwenye mboo yako na kuathiri vibaya mzunguko wa damu wa kusababisha mboo kusimama3. Msongo wa mawazo wa mara kwa mara unaweza pia kusababisha kupungua kwa viwango vya homoni ya testosterone – hali inayoashiria mkwamo.

Hatua ya kumtembelea mtaalamu wa huduma za afya inaweza kusaidia kutatua tatizo linalokusumbua. Kumbuka kuwa hakuna tofauti kati ya kumtembelea daktari kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa moyo wako au mwanasaikolojia au mtaalamu wa tiba ya magonjwa ya akili kwa ajili ya uchunguzi wa akili!

Unyogovu unaweza kusababisha kupungua kwa hamu ya kushiriki ngono na matatizo ya kusisimkwa kabisa. Hata hivyo, kwa upande mwingine, ugonjwa wa ED unaweza kusababishwa na madhara ya baadhi ya dawa za afya ya akili4. Pata ushauri wa daktari wako ili uone iwapo inawezekana kubadilisha dawa unazotumia, na iwapo haiwezekani, unaweza kutumia mojawapo ya matibabu bora ya ugonjwa wa ED yanayopatikana.

[1] Mayo Clinic. Erectile dysfunction. Accessed online: https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/erectile-dysfunction/symptoms-causes/syc-20355776 [2] Harvard Health Publishing. Erectile dysfunction often a warning sign of heart disease. Accessed online: https://www.health.harvard.edu/blog/erectile-dysfunction-often-a-warning-sign-of-heart-disease-201110243648 [3] GoodRx. How Depression and Anxiety Can Lead to Erectile Dysfunction. Accessed online: https://www.goodrx.com/blog/how-depression-and-anxiety-can-lead-to-erectile-dysfunction/ [4] GoodRx. Can medications cause erectile dysfunction?