Kuendelea mbele - Jinsi ya kutibu ugonjwa wa ED
Zungumza na daktari wako
Pata ushauri wa mtaalamu wako wa huduma za afya ili kufutilia mbali uwezekano wa matatizo yoyote ya kimwili ambayo yanaweza kusababisha ugonjwa ED. Habari njema ni kwamba, kuna mabadiliko ya mtindo wa maisha unayoweza kufanya ili kutatua hali ya ED.
Fanya mazoezi
Je, hiyo ni sababu nyingine ya kumwonea wivu huyo jamaa aliyejaza misuli? Bila shaka si tu hali yake ya kujaza misuli inayovutia zaidi… Uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa ED huongezeka kadri uzani wa mwili unapoongezeka (BMI)1, kwa hivyo, ndiyo, uzani wa mwili huchangia.
Kupunguza uzani, kula lishe bora, kuacha kuvuta sigara, kupunguza unywaji wa pombe na mazoezi ya misuli ya upande wa chini wa nyonga zako yanaweza kusaidia kutibu ugonjwa wa ED2. Hakikisha kuwa unafanya mazoezi ya kutembea mara kwa mara: kulingana na utafiti wa chuo kikuu cha Harvard, kutembea kwa dakika 30 kila siku hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa ED kwa asilimia 41 (41%)
Dawa za kumeza/kunywa
Dawa za kumeza/kunywa ni matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa ED kwa sababu ni salama, zinafanya kazi, zina madhara machache na zinapatikana kwa urahisi kwenye duka la dawa lililo karibu nawe. Dawa hizi hufanya kazi kwa kutuliza misuli ya mboo yako, hivyo basi kuongeza mzunguko wa damu ili mboo yako iweze kusimama unaposisimkwa.
[1] National Library of Medicine. Obesity--significant risk factor for erectile dysfunction in men. Accessed online: https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24720114/ [2] Harvard Health Publishing. 5 natural ways to overcome erectile dysfunction. Accessed online: https://www.health.harvard.edu/mens-health/5-natural-ways-to-overcome-erectile-dysfunction [3] Mayo Clinic. Erectile dysfunction: Viagra and other oral medications. Accessed online: https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/erectile-dysfunction/in-depth/erectile-dysfunction/art-20047821